0

Star toka kwa Bongo Fleva, Nay wa Mitego amefunguka na kusema sababu pekee inayomfanya awe kimya kwa hivi sasa ni mipango yake ya kugombea uraisi mwaka 2020.

Nay wa Mitego ni msanii ambaye anajulikana kwa vituko Chake ikiwemo Uwezo wake wa kuwachana watu kwenye jamiii hasa wasanii wenzake kuhusu mambo mbali mbali.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Risasi Vibes, Nay alisema kwa sasa ameamua kujitenga na skendo kwani anajiandaa kugombea urais mwaka 2020 japokuwa hawezi kuweka wazi atagombea kwa chama gani hivyo akaona ni vema aachane na skendo zisizokuwa na maana.

Hivi sasa kumekuwa na trend kubwa ya wasanii mbali mbali kujiingiza Kwenye mambo ya siasa na kugombea nafasi mbali mbali kama vile Wasanii wakongwe wa Bongo fleva Profesa Jay na Sugu ambao wote ni wabunge na Kala ambaye nae alisha tangaza kuja kuingia kwa siasa badae.


Post a Comment

 
Top