0
Baada ya siku   moja toka taarifa ya Msanii Elizabeth michael Lulu kuachiwa gerezani na Kutumikia Kifungo cha nje,kumekuwa na maneno mengi mitandaoni lakini haya hapa ni maneno ya Mama Kanumba baada ya taarifa izo.

mama Kanumba amesema, tangu alipopata tetesi za msanii huyo ametoka jela, amejikuta anakosa usingizi na kuumwa presha.

Ameongeza na kusema, kutokana na suala hilo, imemlazimu leo Jumatatu kwenda kwenye maombi kwa ajili ya afya yake hiyo.

Amesema, licha ya kuwa si yeye aliyemuhukumu, Lulu alipaswa kukaa hata mwaka mmoja ili roho yake iridhike lakini ndio hivyo: "Siku zote maskini hana haki."

Post a Comment

 
Top